Roma,Italia.
HISTORIA nyingine kubwa imeandikwa kwenye mchezo wa soka duniani wikendi hii baada ya Mshambuliaji wa klabu ya Vicenza inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Italia (Seria B),Cristian Galano,kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya kijani.
Galano alionyeshwa kadi ya kijani baada ya kukiri/kusema kuwa mabeki wa Vitrus Entella hawakugusa mpira pale klabu yake ya Vicenza ilipozawadiwa kona na mwamuzi Marco Mainardi.
Mapema mwaka huu mamlaka za juu zinazosimamia ligi ya Seria B ziliamua kuja na kadi ya kijani ikiwa ni jitihada za kuisafisha ligi hiyo ambayo kwa kipindi kirefu imekubwa na kashfa ya upangaji wa matokeo.
Kadi ya kijani hutolewa kama heshima kwa mchezaji anayeonyesha mchezo wa kiungwana yaani Fair Play.
Baadhi ya matukio yanayoonyesha mchezo wa kiungwana ni mchezaji kukataa kufaidika na makosa ya mwamuzi kama kutoa kona,adhabu ama penati kimakosa.Mchezaji wa timu pinzani kutoa mpira nje ama kusimamisha mchezo pale mchezaji wa timu pinzani anapopata tatizo la kuumia na kadhalika.
Katika kufanikisha kuwa kadi ya kijani inapewa uzito wa kipekee imeamuliwa kuwa mchezaji atakayeonyeshwa kadi nyingi zaidi za kijani atatunukiwa tuzo mwishoni mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment