Dar Es Salaam,Tanzania.
Baraza la michezo Tanzania (BMT) limetangaza kujitambua ukodishwaji wa klabu ya Yanga kwa kuwa ni kinyume na katiba ya klabu hiyo.
Katibu mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa mkataba huo kati ya Baraza la Wadhamini wa Yanga na kampuni iliyoikodi klabu hiyo, haukufuata taratibu.
"Ili Yanga iweze kubadili jina na kuitwa Yanga Yetu ni lazima ipite kwa msajili. Wao hawajaenda kwa msajili wanaanza kutangaza jina jipya. Huko ni kupinga katiba," alisema
Kiganja.
0 comments:
Post a Comment