Dar Es Salaam,Tanzania.
Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja,amesema sababu ya wapinzani wao Yanga kumfukuza kocha Hans van der Pluijm ni kutokana na kikosi chao kuongoza ligi.
Mayanja amesema viongozi wa Yanga wanaumia kuiona Simba inaongoza ligi na inapata matokeo mazuri kwenye mechi zao ndio maana wamechanganyikiwa na kuamia kuwatimua makocha wao.
“Hicho wanachokifanya ni sawa na kujichanganya na kuzidi kujipoteza Simba ya msimu huu hawataiweza hata kama watafanya usajili mpya wa wachezaji huu ni mwaka wetu,”amesema Mayanja.
Simba inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 29, huku Yanga ikiwa na pointi 24 katika michezo 11.
0 comments:
Post a Comment