Buenois Aires,Argentina.
LICHA ya kuonyesha kiwango kibovu kabisa katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Peru na Paraguay kocha wa Argentina,Edgardo Bauza,bado ameendelea kuwa na imani na nyota wake Sergio Agüero na Angel Di María baada ya kuwajumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 26 cha nchi hiyo kitakachoshuka dimbani mwezi Novemba kuvaana na Brazil pamoja na Colombia katika michezo ya kusaka tiketi ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.
Aidha Bauza amewatema kikosini nyota kama Erik Lamela, Matías Kranevitter, Marcos Rojo na Mariano Andújar na nafasi zao kuchukuliwa na Gerónimo Rulli,Enzo Pérez Julio Buffarini pamoja na Marcos Acuña huku Lionel Messi akirejea baada ya kukosa michezo miwili iliyopita kutokana na kuwa majeruhi.
Argentina itashuka dimbani Novemba 11 mwaka huku huko Belo Horizonte kucheza na wenyeji wao Brazil kisha siku tano baadae watakuwa nyumbani Buenois Aires kutifuana na Colombia.
Kikosi Kamili:
Makipa: Sergio Romero (Manchester United), Nahuel Guzmán (Tigres), Gerónimo Rulli (Real Sociedad).
Mabeki: Martin Demichelis (Espanyol),Mateo Musacchio (Villarreal), Nicolás Otamendi (Manchester City), Ramiro Funes Mori (Everton), Gabriel Mercado (Sevilla),Facundo Roncaglia (Celta de Vigo), Emanuel Mas (San Lorenzo), Pablo Zabaleta (Manchester City), Julio Buffarini (São Pablo)
Viungo:Javier Mascherano (Barcelona),Guido Pizarro (Tigres Mexico), Lucas Biglia (Lazio), Ever Banega (Inter Milan), Enzo Pérez (Valencia), Nicolás Gaitán (Atlético Madrid),Angel Di María (Paris Saint-Germain),Marcos Acuña (Racing)
Washambuliaji: Angel Correa (Atlético Madrid),Lionel Messi (Barcelona), Paulo Dybala (Juventus), Gonzalo Higuaín (Juventus),Sergio Agüero (Manchester City), Lucas Pratto (Atlético Mineiro)
0 comments:
Post a Comment