London,England.
MESUT OZIL (Pichani) usiku huu amefunga mabao matatu (Hat- Trik) na kuiwezesha Arsenal kuichapa Ludogoretes mabao 6-0 katika mchezo wa kundi A wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Alexis Sanchez, Theo Walcott na Alex Oxlade Chamberlain.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la A,Paris Saint Germain ikiwa nyumbani Parc des Princes imeifumua FC Basel ya Uswisi mabao 3-0.Shukrani kwa mabao Angel Di Maria,Lucas Moura na Edinson Cavani.
0 comments:
Post a Comment