728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 14, 2016

    Gerard Pique sasa autaka Urais



    Barcelona, Ufaransa.

    BAADA ya mapema wiki hii kufichua kuwa atastaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Hispania mara tu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 zitakapokuwa zimekwisha,beki wa kati wa Barcelona,Gerard Pique,amesema kuwa anatamani siku moja aje kuwa rais wa klabu hiyo yenye maskani yake katika jimbo la Catalunya.

    Pique mwenye umri wa miaka 29 sasa amesema hafikirii kabisa kufuata nyayo za akina Pep Guardiola na Luis Enrique ambao baada ya kustaafu soka waliamua kuwa makocha,badala yake anatamani kuwa rais wa Barcelona.

    Akijibu swali aliloulizwa na kituo cha televisheni cha TV3 cha Hispania kama kweli ana ndoto ya kuwa rais wa Barcelona hapo siku za usoni ama ni utani/geresha tu,Pique amesema kuwa kila anapotamka jambo huwa amemaanisha.

    "Ndio,Ninapotamka jambo huwa nimemaanisha.Nataka kuwa rais wa Barcelona.Ni wadhifa/ngazi ninayotaka kuwa nayo pindi nitakapostaafu kucheza soka.

    Sijioni kama naweza kuwa kocha/meneja.Sidhani kama nitafurahia wadhifa huo.Kama rais nitaweza kufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya klabu hii niipendayo.Siku moja safari yangu ya kucheza soka itafikia mwisho na hatua nitakayopenda kuichukua ni kuwa rais wa Barcelona.









    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Gerard Pique sasa autaka Urais Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top