728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 29, 2016

    Ligi kuu bara:Michezo mitano kupigwa leo,miwili kesho


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itaendelea siku ya leo Jumamosi Oktoba 29, mwaka huu kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili—michezo yote ikiwa ni ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa kwanza.

    Leo Kagera Sugar inacheza dhidi ya Azam FC katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati kesho itakuwa ni zamu ya Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenyeUwanja wa CCM Kirumba.

    Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

    Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

    Kesho Jumapili Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi kuu bara:Michezo mitano kupigwa leo,miwili kesho Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top