ARGENTINA ikiwa ugenini Lima imeshindwa kutamba baada ya asubuhi hii kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji Peru katika mchezo mkali wa kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko nchini Urusi.
Ramiro Funes Mori alianza kuiandikia Argentina bao la kuongoza dakika ya 15 ya mchezo kutokana na mpira wa kona wa Paul Dybala.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili wenyeji Peru walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 58 kupitia kwa nahodha wao Paolo Guerrero.Bao hilo halikudumu sana kwani mnamo dakika ya 77 ya mchezo Gonzalo Higuaín aliifungia Argentina bao la pili.
Mchezo ukiwa unaelekea ukingoni madhambi ya mlinzi Ramiro Funes Mori yaliyofanywa kwa Paolo Guerrero yaliizawadia Peru penati iliyofungwa kwa ustadi mkubwa na Christian Cueva katika dakika ya 84' na kufanya mchezo uishe kwa sare ya mabao 2-2.
Matokeo Mengine
Ecuador 3 - 0 Chile
Uruguay 3 - 0 Venezuela
Paraguay 0 - 1 Colombia
Brazil 5 - 0 Bolivia
Peru 2 - 2 Argentina
0 comments:
Post a Comment