Abidjan,Ivory Coast
IVORY COAST imeianza vyema mikikimikiki ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi kwa ukanda wa Afrika baada ya usiku huu kutoka nyuma na kuifumua Mali kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa kundi C uliochezwa katika dimba la uwanja wa Stade Bouaké huko Abidjan.
Mali ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 18 ya mchezo kupitia kwa Sombotou Yabatare.
Bao hilo halikudumu sana kwani katika dakika ya 26,Kodja Jonathan,aliifungia Ivory Coast bao la kusawazisha kwa mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Mali, Ssisoko na kutinga wavuni.
Salif Coulibary aliiandikia Ivory Coast bao la pili baada ya kujifunga katika dakika ya 31 akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.Gervinho aligongelea msumali wa mwisho katika jeneza la Mali baada ya kuifungia Ivory Coast bao la tatu katika dakika ya 34 ya mchezo.
Katika mchezo mwingine wa kundi C,Gabon ikiwa nyumbani imebanwa mbavu na Morocco na kulazimishwa kutoka sare ya bila kufungana.
Congo DR ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Stade des Martyrs ulioko Kinshasa imeichapa Libya mabao 4-0 katika mchezo wa kundi A.
Mabao ya Congo DR yametiwa kimiani na Dieumerci Mbokani aliyefunga mara mbili huku Jonathan Bolingi na Firmin Mubele wakifunga mara moja moja.
Kundi D:Senegal ikiwa nyumani Dakar imeifunga Cape Verde kwa mabao 2-0.Shukrani kwa mabao ya dakika za 25 na 80 ya Nabir Keita pamoja na Moussa Sow.
0 comments:
Post a Comment