728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 15, 2016

    Huyu ndiye Lionel Messi:Bao moja rekodi moja kubwa.


    Barcelona,Hispania.

    Lionel Messi ameendelea kuvunja rekodi zilizokuwepo zamani na kuweka zake hii ni baada ya jioni ya leo kuweka rekodi nyingine mpya.

    Messi,28,ambaye alikuwa nje kwa siku 21 akiuguza jeraha la mguu leo ametumia dakika tatu tu tangu aingie uwanjani na kuifungia Barcelona bao moja na kuiwezesha kuifunga Deportivo la Coluna mabao 4-0 nyumbani Camp Nou.

    Kwa kufunga bao hilo moja Messi amefikisha mabao 180 katika michezo 176 ya La Liga katika uwanja wa Camp Nou na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengine zaidi katika uwanja wa nyumbani.

    Awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ( Telmo Zarraonandía Montoya) wa Atletico Bilbao aliyefariki 23 Februari 2006.

    ..

    .


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Huyu ndiye Lionel Messi:Bao moja rekodi moja kubwa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top