728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 21, 2016

    Mwamuzi aliyemlima kadi nyekundu Xhaka aondolewa ligi kuu England.


    London,England.

    MWAMUZI Jon Moss ameondelewa kwenye orodha ya waamuzi watakaokaochezesha michezo ya ligi kuu nchini England wikendi hii.

    Moss ameondolewa kwenye orodha hiyo ikiwa ni adhabu ya kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za soka baada ya Jumamosi iliyopita kumtoa kimakosa kwa kadi nyekundu kiungo wa Arsenal Granit Xhaka.

    Xhaka,24,alionyeshwa kadi nyekundu na kutolewa nje katika dakika ya 70 baada ya kumkwatua kwa nyuma winga wa Swansea City,Modou Barrow.Uamuzi huo umetafsiriwa kuwa ulifanyika kimakosa na badala yake kiungo huyo alipaswa aonyeshwe kadi ya njano.


    Wakati Moss akikumbana na adhabu hiyo ya kukosa michezo ya wikendi hii ,Xhaka yeye ataendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu ya ligi kuu England kama ilivyokuwa imeamuliwa hapo awali.

    Moss atachezesha mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini England kati ya Sheffield United na Bradford utakaochezwa siku ya Jumamosi saa 11 jioni.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mwamuzi aliyemlima kadi nyekundu Xhaka aondolewa ligi kuu England. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top