728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 28, 2016

    Babu Pluijm arejea Yanga SC




    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Hatimaye uongozi wa klabu ya Yanga SC umeamua kumrejesha kocha wake Hans Van Der Pluijm kuendelea na nafasi yake ya ukocha mkuu katika klabu hiyo, ikiwa ni siku siku tano tu tangu aandike barua ya kujiuzuru.

    Hayo yamefikiwa leo baada ya kikao cha pamoja kati ya uongozi wa klabu ya Yanga na Hans Van der Pluijm kilichofanyika katikati ya jiji la Dar es salaam na kufikia muafaka wa mdachi huyo kuendelea na kandarasi yake.

    Kocha Hans raia wa Uholanzi aliyeishi Afrika kwa miaka zaidi ya 18, aliandika barua ya kujiuzuru siku ya jumatatu, kufuatia kutofurahishwa na kitendo cha uongozi wa klabu ya Yanga kumleta kocha wa Zesco George Lwandamina na kufanya nae mazungumzo ya kuchukua nafasi yake bila kumshirikisha.

    Mtazamo wa wapenzi, wanachama wa klabu hiyo ulikua tofauti na zaidi ukipinga kuondolewa kwa kocha huyo, ili hali rekodi yake ikiwa ni ya kiwango cha juu katika michuano ya Ligi ya Kuu Tanzania, Kombe la FA, na Kombe la Shirikisho Afrika.

    Uongozi baada ya kuona haukumtendea haki kocha Hans, leo umekutana na kocha huyo na kufikia muafaka wa kumrejesha kazini kuendelea na kibarua chake.

    Kurejea kazini kwa Hans kunamanisha mipango ya kumleta kocha George Lwandamina kuchukua mikoba yake mwezi ujao kusitishwa, na sasa uongozi umeahidi kumpa ushirikiano wote kocha Hans katika kuhakikisha anatetea Ubingwa wa Ligi, Kombe la FA na katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Babu Pluijm arejea Yanga SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top