London,England.
WINGA wa Chelsea Victor Moses ameendelea kumshambulia kwa maneno kocha wake wa zamani Mreno Jose Mourinho baada ya kudai kuwa kocha huyo alikuwa na wachezaji wake ndiyo maana alikuwa akimtoa kwa mkopo kila mara bila kumweleza sababu.
Moses mwenye umri wa miaka 25 sasa ametoa kauli hiyo jana Ijumaa wakati akifanya mahojiano na ESPN FC.
"Hakuwa akiongea na mimi. Moses ameiambia ESPN FC wakati akijibu swali aliloulizwa kama alikuwa akielezwa sababu ya kutolewa kwa mkopo kila mara.
"Nilikuwa nikijiuliza kwanini ananitoa kwa mkopo kila wakati.Nikahisi tayari ana wachezaji wake.Alisema Moses ambaye katika misimu mitatu iliyopita amecheza kwa mkopo katika vilabu vya Liverpool, Stoke City na West Ham.
Wakati huo huo Moses amemwagia sifa kemkem kocha wake mpya Muitaliano Antonio Conte baada ya kumpa nafasi nyingine ya kuonyesha kipaji chake ndani ya klabu yake ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment