Manchester,England.
Unaweza kudhani kuwa ni utani au mzaha toka kwa kocha wa zamani Manchester United Alex Ferguson juu ya jinsi alivyofikia uamuzi wa kumsajili gwiji wa Kifaransa Eric Cantona.
Ferguson kutoka katika kitabu chake kiitwacho Leading amefichua kwamba alimsajili Cantona baada ya kusikiliza mazungumzo (uchambuzi) yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wake Steve Bruce na Gary Pallister wakati wakioga baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Leeds United mwaka 1992.
Cole na Cantona
Anasema "Niliamua kuungana na wachezaji wangu kuoga pamoja kitu ambacho hakikuwa kawaida yangu kufanya hiyo.Nilikuwa nikifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Bruce na Pallister kuhusu mchezo tuliokuwa tumetoka kuucheza.Wote wawili walikuwa wakisifia mchezo mzuri ulionyeshwa na Cantona ambaye ndiyo kwanza alikuwa amejiunga na Leeds Akitokea Nimes.Alimaliza Ferguson
Pallister na Cantona wakiwa na taji la FA
Cantona aliifungia Manchester United jumla ya mabao 82 katika michezo 185 baada ya kudumu kwa miaka mitano huku akitwaa mataji manne ya ligi kuu pamoja na mataji ya FA.
Cantona akimchapa kiatu shabiki aliyemtusi |
0 comments:
Post a Comment