Harare,Zimbabwe.
TIMU ya taifa ya Zimbambwe imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON mwakani nchini Gabao baada ya jioni ya leo kuifunga Malawi kwa mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi L uliochezwa katika uwanja wa taifa uliopo jijini Harare.
Mabao ya Zimbabwe katika mchezo wa leo yamefungwa na Knowledge Musona (16),Khama Billiat (37) na Cuthbert Malajila (88).
Kwa matokeo hayo Zimbabwe inayofundishwa na kocha Kalisto Pasuwa imefuzu baada ya kujikusanyia pointi 11 huku washindani wake wa karibu Guinea wakipoteza baada ya kufungwa 1-0 na Swaziland huko Mbabane.
0 comments:
Post a Comment