728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 06, 2016

    AZAM ACADEMY MABINGWA AYC,KAPOMBE BEKI BORA WA MICHUANO

    Dar es Salaam,Tanzania.

    TIMU ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam FC Academy’, usiku wa jana
    imefanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki ‘Azam Youth Cup 2016’
    baada ya kuichapa Ligi Ndogo Academy kutoka Kenya mabao 3-0,mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex.

    Azam Academy inatwaa ubingwa huo ikiwa imefikisha jumla ya pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza nyingine zikiwa dhidi ya
    Future Stars Academy kutoka Arusha (4-1) na Football for Good Academy
    ya Uganda (5-1).

    Shujaa wa mabingwa hao kwenye mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wake hatari Shaaban Idd
    aliyepachika wavuni mabao mawili kwa ustadi mkubwa dakika ya 15 na jingine 90, alilolifunga kwa staili ya
    ‘tik-tak’ huku bao jingine likifungwa na mshambuliaji mwingine hodari wa timu hiyo Yahaya Zaidi, katika dakika ya 27.

    Shaaban kufunga mabao hayo kunamfanya awe amefikisha matano na kuibuka mfungaji bora wa
    michuano hiyo huku Yahaya aliyekuwa akimfukuzia kwa kasi akiwa nayo manne.

    Ligi Ndogo waliopoteza pambano hilo wenyewe wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu nyuma ya Football for Good Academy waliokamata nafasi ya pili
    huku Future Stars ikishika nafasi ya nne, timu zote hizo zikiwa zimekisanyia jumla ya pointi tatu lakini zimetofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa (GD).

    Tuzo binafsi zatolewa
    Wakati Azam Academy ikiibuka mabingwa, pia baadhi ya wachezaji
    waliofanya vizuri kwenye kila idara waliweza kupewa tuzo binafsi kufuatia
    mafanikio hayo.

    Mshambuliaji wa Azam Academy Shaaban aling’ara katika utoaji tuzo
    hizo baada ya kutwaa tuzo mbili, ile ya ufungaji bora na mshambuliaji bora wa michuano hiyo baada ya kuwa kinara wa mabao akipachika matano huku Tuzo ya Beki Bora ikienda kwa beki wa Azam Academy, Abas Kapombe, ambaye ni mdogo wa staa wa Azam FC, Shomari Kapombe.

    Tuzo ya Mchezaji Bora wa michuano hiyo imeenda kwa Stephen Bongomin
    wa Football for Good Academy na staa mwingine wa timu hiyo Allan Ganukupa, alitwaa Tuzo ya Kiungo Bora wa michuano hiyo huku ile ya Kipa Bora ikibebwa na Rodgers Siteti.

    Michuano hiyo iliyoandaliwa na Azam FC ni ya kwanza kufanyika nchini,ambapo itakuwa endelevu na itafanyika tena mwakani ikihusisha academy za nchi za Afrika Mashariki lengo ni kukuza kiwango cha soka cha nchi hizo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM ACADEMY MABINGWA AYC,KAPOMBE BEKI BORA WA MICHUANO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top