Arizona,Marekani.
TIMU ya taifa ya Uruguay ikiwa bila ya nyota wake Luis Suarez imeianza vibaya michuano ya kumsaka bingwa wa kombe la Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kufungwa mabao 3-1 na timu ya taifa ya Mexico katika mchezo mkali wa kundi C uliochezwa katika uwanja wa University
of Phoenix Stadium huko Arizona,Marekani.
Jahazi la Uruguay lilianza kwenda kombo dakika ya 4 tu ya mchezo baada ya mlinzi wake Alvaro Perreira kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.
Dakika ya 74 nahodha Diego Godin aliisawazishia bao Uruguay ambalo halikuwa na msaada sana kwani Mexico walikuja juu na kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Rafa Marquez dakika ya 85 na Hector Herrera dakika ya 90 na kufanya mchezo uishe kwa Mexico kushinda kwa mabao 3-1dhidi ya Uruguay.
KADI NYEKUNDU
Mexico na Uruguay zililazimika kumaliza mchezo zikiwa na wachezaji pungufu baada ya wachezaji wao kulimwa kadi nyekundu kwa michezo mibaya.Matias Vecino 45' kwa Uruguay na Andres Guardado 73' kwa Mexico.
VIKOSI
México: Talavera; Araujo, Reyes, Moreno,
Layún; Herrera, Márquez, Guardado;Aquino, Hernández, Corona.
Uruguay: Muslera; M.Pereira, GodÃn,
Giménez, A.Pereira; C.Sánchez, A.RÃos,
Vecino, Rolan; Lodeiro, Cavani.
Katika mchezo wa mapema wa Kundi C uliochezwa katika uwanja wa jeshi, Chicago, Illinois ,Venezuela ilichomoza na ushindi baada ya kuilaza Jamaica kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 15 na Josef Martinez baada ya kupokea pasi maridadi toka kwa Alejandro Guerra. Dakika ya Jamaica ilipata pigo baada ya mlinzi wake Rudolf Austin kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
0 comments:
Post a Comment