Cagliari,Italia.
KIUNGO wa Pescara Mghana, Sulley Muntari usiku wa kuamkia leo alilazimika kususia mchezo na kuamua kutoka uwanjani kabla ya wakati baada ya kukasirishwa na lugha za kibaguzi alizokuwa akitolewa na mashabiki wa Cagliari katika mchezo wa ligi ya Seria A ulioisha kwa timu yake kulala kwa bao 1-0.
Tukio hilo limetokea huko Stadio Sant'Elia,ambapo mashabiki wa Cagliari wakionyesha kukosa ustaarabu walikuwa wakitoa lugha za kibaguzi kila mara Muntari,32, alipokuwa akishika mpira.
Baada ya kuona uzalendo unamshinda Muntari alimfuata mwamuzi,Daniele Minelli pamoja na msaidizi wake kutoa malalamiko yake ili mchezo usimamishwe kama taratibu zinavyoagizwa lakini aliambulia kulimwa kadi ya njano akionekana kuwa ni msumbufu.
Akiwa amejaa jazba Muntari aliamua kususia mchezo na kutoka uwanjani akiiacha Pescara akibaki wa wachezaji kumi (10).
0 comments:
Post a Comment