728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, December 04, 2015

    BARCA YATANGAZA SILAHA 23 TAYARI KWA KLABU BINGWA YA DUNIA,MSN NDANI.

    Barcelona,Hispania.

    Barcelona imetangaza nyota 23 watakaoiwakilisha katika michuano ya kuwania taji la vilabu bingwa duniani inayotarajiwa kuanza Desemba 10 mpaka 20 nchini Japan.

    Katika kikosi hicho kilichotangazwa jana alhamis kocha wa timu hiyo Muhispania Luis Enrique amewajumuisha washambuliaji wake wanaotesa duniani kwasasa wakijulikana kama (MSN) ikiwa na maana ya Messi,Suarez na Neymar.

    Pia Enrique amewajumuisha katika kikosi hicho makinda Sergi Samper, Gerard Gumbau, Munir na Sandro Ramirez.

    Barcelona inatarajiwa kuanzia hatua ya nusu fainali kwa kuvaana na Club America ama Guangzhou
    Evergrande siku ya Disemba 17 na iwapo itafuzu itavaana na River Plate katika fainali itakayopigwa Desemba 20 huko Yokohama.

    KIKOSI KAMILI

    Walinda mlango: Marc-Andre Ter Stegen,Claudio Bravo, Jordi Masip.

    Walinzi: Jordi Alba,Douglas, Gerard Pique, Javier Mascherano, Marc Bartra,Dani Alves, Adriano, Thomas Vermaelen,Jeremy Mathieu.

    Viungo: Ivan Rakitic, Sergio
    Busquets, Andres Iniesta, Sergi Roberto,Sergi Samper, Gerard Gumbau.

    Washambuliaji: Luis Suarez, Neymar, Lionel Messi, Munir, Sandro Ramirez.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCA YATANGAZA SILAHA 23 TAYARI KWA KLABU BINGWA YA DUNIA,MSN NDANI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top