Addis Ababa,Ethiopia.
Timu za taifa za Rwanda na Uganda zimefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Cecafa Chalenji Cup baada ya leo jioni kuibuka na ushindi katika michezo yao ya nusu fainali.
Uganda ambao ni mabingwa mara 14 wa michuano hiyo wametinga fainali baada ya kuwafunga wenyeji Ethiopia kwa penati 5-3 baada ya kwenda nao sare ya 0-0 ndani ya dakika 120.
Penati zilizoipeleka fainali Uganda zimefungwa na Muzamiru Mutyaba, Denis
Okot, Isaac Muleme, Joseph Ochaya na nahodha Faruku Miya.
Katika mchezo mwingine Rwanda nayo imefuzu kwa staili ya Uganda baada ya kuichapa Sudan kwa penati 4-2 kufuatia sare ya goli 1-1 katika muda wa kawaida.
Kufuatia matokeo hayo Rwanda na Uganda zitavaana siku ya jumapili kumsaka bingwa mpya wa michuano hiyo huku Sudan na Ethiopia zenyewe zikichuana kugombea nafasi ya tatu na ya nne.
0 comments:
Post a Comment