728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 03, 2015

    FIFA YAJA NA MPANGO MPYA KOMBE LA DUNIA,STARS HUENDA IKAPATA SHAVU

    Zurich,Uswisi.


    Shirikisho la vyama vya soka duniani FIFA lenye makao makuu yake Geneva,Uswisi limeripotiwa kuja na mpango wa kuiboresha zaidi michuano ya kombe la dunia.

    Habari za kuamini ambazo zimeifikia sokaextra.blogspot.com kutoka Uswisi zinadai kuwa leo siku ya alhamis FIFA itakuwa na mkutano wake jijini Zurich ambapo pamoja na masuala mengine FIFA itazungumzia mpango wa kuongeza timu shiriki za kombe la dunia kutoka 32 za sasa mpaka 40.

    Fog covers FIFA's headquarters in Zurich on December 3, 2015

    Iwapo mpango huo utakubaliwa basi kombe la dunia la mwaka 2026 litashudia timu 40 zikitoana jasho huku jumla ya michezo 96 ikipingwa kumpata bingwa wa taji hilo kubwa zaidi duniani kwa mchezo wa soka.

    Ina aminika kuongezeka kwa timu shiriki kutatoa mwanya kwa mataifa kama Tanzania kuweza kupata nafasi katika michuano hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FIFA YAJA NA MPANGO MPYA KOMBE LA DUNIA,STARS HUENDA IKAPATA SHAVU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top