728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 03, 2015

    USAJILI:AGUERO AGOMEA MKATABA MPYA MAN CITY ATAJA SIKU YA KUONDOKA,WENGER AIOMBA BODI IMSAIDIE AMPATE STONES,MOURINHO KURUDI HISPANIA



    Aguero:Sergio Aguero27 amesema hatasaini tena mkataba mpya wa kuichezea Manchester City na badala yake atajiunga na Independiente ya kwao Argentina pindi mkataba wake wa sasa Etihad utakapofika mwisho hapo mwaka 2019.

    Semedo:Vilabu vya Manchester City, Chelsea na Arsenal kwa pamoja vimeripotiwa kutaka kumsajili mlinzi wa kulia wa Benfica Nelson Semedo,22.(O Jogo)

    Nouri:Arsenal na Manchester United vimeingia katika vita ya kuisaka saini ya kiungo kinda mwenye kipaji toka Ajax Abdelhak Nouri.(Star)

    Cheryshev:Liverpool iko tayari kufungua mazungumzo kwa ajili ya kumsajili winga wa Real Madrid Denis Cheryshev,24.(Fichajes.com)

    Stones:Arsene Wenger ameiomba bodi ya Arsenal ifanye juu chini ili kuhakikisha inamsajili mlinzi kinda wa  Everton John Stones,21 ili kukiimarisha kikosi chake ambacho kimeendelea kukumbwa na wimbi la majeruhi.(Fichajes.com)

    Mourinho:Klabu ya Valencia imeripotiwa kujipanga kumnasa kocha Jose Mourinho katika majira yajayo ya joto ya usajili licha ya siku ya jana jumatano kumteua Gary Neville kuwa kocha wake wa muda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:AGUERO AGOMEA MKATABA MPYA MAN CITY ATAJA SIKU YA KUONDOKA,WENGER AIOMBA BODI IMSAIDIE AMPATE STONES,MOURINHO KURUDI HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top