London,England.
Ni rasmi kuwa Santiago "Santi" Cazorla, atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati akiichezea Arsenal katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Norwich City ambapo matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.
Wachambuzi wengi wa soka duniani baada ya kupata taarifa hizi mbaya wameanza kuiondoa taratibu Arsenal katika kinyang'anyiro cha taji la ligi kuu wakisema kuwa nyota huyo wa kiungo ni muhimu sana na Arsenal imekuwa ikipata matokeo mazuri pindi anapokuwa dimbani.
Hoja yao (waliyoiita sababu 2197) ni kuwa Arsenal inapokuwa na Cazorla katika kikosi chake imefanikiwa kushinda asilimia 62 ya michezo yake na kutoka sare kwa asilimia 20.Lakini inapocheza bila ya kiungo huyo Arsenal imefanikiwa kushinda jumla ya asilimia 20 tu ya michezo yake huku ikitoka sare kwa asilimia 60.
Michezo ambayo Arsenal itacheza bila ya Cazorla:fOlympiakos (December 9), Manchester City ( December 21), Liverpool (Januari 13), Chelsea (January 24) na Manchester United (February 27)

0 comments:
Post a Comment