Real Madrid inakabiliwa na hatari ya kutupwa nje ya michuano ya kombe la Copa del Rey kwa kosa la kumchezesha mchezaji aliyekuwa amefungiwa.
Real Madrid ambayo jana jumatano ilishuka dimbani El Carranza kuvaana na Cadiz na kupata ushindi wa magoli 3-0 ilimchezesha kwa makosa winga wake Denis Cheryshev aliyepaswa awe nje ya mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano alizozipata msimu uliopita akiichezea kwa mkopo Villarreal.
Cheryshev,25 raia wa Urusi katika mchezo dhidi ya Cadiz aliifungia Real Madrid goli la kuongoza kabla ya kutolewa nje wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Mateo Kovacic baada ya mashabiki kuanza kupiga kelele na kumwambia Rafael Benitez kuwa mchezaji huyo amefungiwa na kwa ushahidi atazamae habari hiyo katika ukurasa wa twitter wa chama cha soka.Baada ya kelele hizo Benitez aliamua kumtoa mchezaji huyo.
Kufuatia tukio hilo Real Madrid inatarajiwa kukumbana na adhabu ya kutolewa mashindanoni kama ilivyokuwa kwa Osasuna msimu uliopita baada ya kumchezesha Unai Garcia aliyekuwa na adhabu katika mchezo dhidi ya Mirandes
0 comments:
Post a Comment