728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 03, 2015

    KERR ATUMBUA MAJIPU SIMBA


    WAKATI Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ‘akitumbua majipu’ ya ufisadi na rushwa serikalini, kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr naye yuko bize ‘akitumbua majipu’ ya kukosa pumzi na stamina ambayo yamekuwa yakikitesa kikosi timu hiyo kwa misimu mitatu.
    Simba imekuwa na tatizo la kushindwa kucheza kwa kasi ile ile ya juu kwa dakika 90 hasa pale inapocheza mechi ngumu kama dhidi ya Yanga au Simba, tatizo ambalo Kerr ameamua kulimaliza kabla ya kukutana na Azam baada ya mapumziko kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
    Miamba hiyo ya Msimbazi mara nyingi imekuwa ikianza mechi zake kwa kasi, lakini huonekana kuchoka kadiri mechi inavyoelekea mwisho na kuwapa nafasi wapinzani kutawala mchezo.
    Ili kulimaliza tatizo hilo kabla ya mechi dhidi na Azam, Kerr ameamua kutumia muda mwingi wa mazoezi ya timu hiyo kuwakimbiza kwa muda mrefu wachezaji wake, ili kuwarudisha stamina na pumzi ndani ya kikosi chake.
    Simba ambayo imeweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na pambano hilo, imekuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume kujiweka sawa kwa ajili ya pambano hilo muhimu kwao msimu huu.
    (CHANZO:GAZETI LA BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KERR ATUMBUA MAJIPU SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top