Birmingham, England.
Kocha wa Aston Villa Mfaransa Remi Garde amesema atakuwa ni mwenye furaha kuikaribisha Arsenal pamoja na mashabiki wake katika uwanja wa Villa Park jumapili ya leo lakini ameonya kuwa uswahiba wake na miamba hiyo ya London utakoma kabla ya mchezo kuanza na kurejea tena baada ya dakika tisini kuwa zimekwisha.
Garde,49 aliyewahi kuichezea Arsenal mwaka 1996-1999 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu England msimu wa 1997/98 amekiri kuwa na mapenzi makubwa na Arsene Wenger lakini amesema atajisahaulisha hilo na kuhakikisha Aston Villa inaibuka na ushindi katika mchezo wa leo.
Akiongea na AVTV,Garde amesema "Nilifurahia kila dakika niliyokuwa na Arsenal.Kuwa upande pinzani na Arsenal ni jambo jipya.Nawakaribisha Villa Park lakini wanapaswa kujua mchezo utakapoanza tu uswahiba wangu kwao utakuwa umekufa mpaka hapo mchezo utakapokuwa umekwisha"
0 comments:
Post a Comment