Dakar,Senegal.
Timu ya taifa ya Nigeria ya U23 imetwaa ubingwa wa michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuilaza timu ya taifa ya Algeria ya U23 kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa usiku wa kuamkia leo huko Dakar,Senegal katika dimba la Leopold Sedar Senghor.
Magoli yaliyoipa ushindi Nigeria yalipatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wake Oghenekaro Etebo huku Algeria wao wakipata goli lao baada ya mlinzi wa Nigeria Segun Oduduwa kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa.
Nigeria itabidi wampongeze kipa wao Emmanuel Daniel kwani katika kipindi cha pili cha mchezo aliwanyima bao Algeria baada ya kudaka penati ya Zinedine
Ferhat.
Kufuatia ushindi huo Nigeria inaungana na Algeria na Afrika Kusini kuiwakilisha Afrika katika michuano ya Olympic itakayopigwa mwakani huko Rio de Janeiro,Brazil.
0 comments:
Post a Comment