Vargas:Klabu ya Arsenal imefungua mazungumzo na klabu ya Napoli kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Mchile Eduardo Varga mwenye thamani ya €16m (£11.3m).(Mediaset)
De Vrij:Kocha wa Manchester United Mdachi Louis Van Gaal ameripotiwa kufikiria kumsajili mlinzi wa Lazio Stefan De Vrij ikiwa atashindwa kumsajili mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos.(Teregraph)
Robinho:Winga Mbrazil Robinho yuko mbioni kutua katika klabu ya Guangzhou Evergrande ya China hii ni siku chache baada ya Mbrazil mwenzake Paulinho kutua klabuni hapo kwa ada ya £9.9m.Guangzhou inafundishwa na kocha Mbrazil Felipe Scolari.(Sky Sports)
Cambiasso:Klabu ya Aston Villa inataka kumsajili kiungo mkongwe Esteban Cambiasso baada ya nyota huyo kumaliza mkataba katika klabu ya Leceister City.(The Sun)
Hamsik:Klabu ya Manchester City inataka kumsajili kiungo wa klabu ya Napoli Marek Hamsik baada ya kuripotiwa kuandaa kitita cha £20m ili kumnasa nyota huyo mwenye miaka 27.(The Sun)
Benteke:Mshambuliaji Christian Benteke anajiandaa kukataa kuhamia Tottenham ili kulazimisha kutua Liverpool hata kama Aston Villa itafikia makubaliano na klabu hiyo ya London.(Evening Standard)
Ekotto:Benoit Assou -Ekotto amejiunga na klabu ya Saint Etienne ya Ufaransa baada ya mapema mwaka huu kutumwa na klabu ya Tottenham.
Young:Ashley Young amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kusalia Manchester United.Mkataba huo utamuwezesha Young kuvuna mshahara wa £120,000 kwa wiki.(The Sun)
Pato:Alexander Pato huenda akarudi tena Ulaya baada ya klabu ya Lazio kuripotiwa kuandaa kitita cha £5.5m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan.(Transfer Talk)
Costa:Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kumsajili winga wa Shakhtar Donetsk Mbrazil Douglas Costa kwa kitita cha €30m.Costa amesaini mkataba wa miaka mitano na kupewa jezi namba 11
0 comments:
Post a Comment