Dar es salaam,Tanzania.
Nahodha na beki wa kati wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ametangaza rasmi kuwa, atastaafu kuichezea timu hiyo miaka mitatu ijayo.
Kauli huyo, aliitoa jana Alhamisi mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake ya Yanga kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar.
Mara baada ya Stars kufungwa na Algeria mabao 7-0, kuliibuka maneno kuwa Cannavaro na beki mwenzake wa kati, Kelvin Yondani, wanaonekana kuchoka kutokana na umri kuwatupa mkono.
Cannavaro amesemakuwa umri wake siyo mkubwa kiasi cha yeye kustaafu kuichezea Stars.
“Hizo kejeli na maneno ya watu nimeyazoea muda mrefu sana, kuhusiana na kiwango changu kushuka na umri kuwa mkubwa, hivyo ninachofanya ni kunyamaza tu.
“Muda wa kustaafu bado haujafika, nitafikiria hivyo miaka mitatu ijayo na tena nikistaafu hapo nitaendelea kuichezea Yanga, ikitokea nimeondoka Yanga basi jua kuwa ndiyo mwisho wangu wa soka umefika kwa sababu sifikirii kuichezea klabu nyingine mara baada ya hapo,” alisema Cannavaro ambaye ni nahodha wa Yanga.
0 comments:
Post a Comment