Addis Ababa,Ethiopia.
Timu za taifa za Rwanda na Uganda jumamosi ya leo zinatarajiwa kushuka katika dimba la Addis Ababa nchini Ethiopia katika mchezo wa fainali ya 38 wa kuwania ubingwa CECAFA Chalenji Cup.
Mchezo huo utakaochezwa mishale ya saa 10:00 jioni kwa saa za Tanzania unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kwani mshindi wa mchezo wa leo atapata kikombe na zawadi ya dola elfu 30,000.
Uganda inaingia katika mchezo wa leo ikiringia rekodi yake nzuri mbele ya Rwanda.Uganda na Rwanda zimekutana mara 29,Uganda imeshinda michezo 15,Rwanda 8 na kutoka sare mara 6.
Kabla ya mchezo wa fainali pia kutakuwa na mchezo wa kumpata mshindi wa tatu na wa nne ambapo wenyeji Ethiopia watavaana na Sudan saa 8:00 mchana.
Timu ziliyotwaa ubingwa mara nyingi zaidi.
Uganda ndiyo timu inayoongoza kwa kutwaa taji la CECAFA mara nyingi zaidi,mpaka sasa imetwaa mara 13,ikifuatiwa na Kenya iliyotwaa mara 6.
Mabingwa wa michuano hiyo kuanzia mwaka 1999.
1999: Rwanda B
2000: Uganda
2001: Ethiopia
2002: Kenya
2003: Uganda
2004: Ethiopia
2005: Ethiopia
2006: Sudan
2007: Sudan
2008: Uganda
2009: Uganda
2010: Tanzania
2011: Uganda
2012: Uganda
2013: Kenya
0 comments:
Post a Comment