728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 02, 2015

    GARY NEVILLE KOCHA MPYA VALENCIA

    Valencia,Hispania.

    Mlinzi na nahodha wa zamani wa Manchester United na England Gary Neville ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Valencia akichukua nafasi ya Mreno Nuno Espirito Santo aliyeachia ngazi kwa hiyari siku ya jumapili usiku baada ya Valencia kulala kwa goli 1-0 toka kwa Sevilla.

    Neville ambaye alikuwa akifanya kazi ya uchambuzi kwenye kituo cha luninga cha Sky Sports huku pia akihudumu kama kocha msaidizi wa England ataungana na ndugu yake Phil Neville kuhakikisha Valencia inafanya vizuri katika ligi ya La Liga kwani mpaka sasa Valencia iko nafasi ya sita ikiwa imefanikiwa kushinda michezo 5 pekee kati ya 13 iliyocheza msimu huu.

    Valencia wamempa Neville mkataba wa kuinoa timu hiyo hadi June 30,2016 huku kukiwa na uwezekano wa kupewa mkataba wa kudumu ikiwa ataonyesha mafanikio.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GARY NEVILLE KOCHA MPYA VALENCIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top