728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 02, 2015

    LEWANDOWSKI AINGIA KWENYE KITABU CHA MAAJABU YA DUNIA




    Mshambuliaji wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Robert Lewandowski ameingia katika headlines baada ya kuweka rekodi nyingine iliyoingia katika kitabu cha Guinness World RecordsRobert Lewandowski ambaye amekabidhiwa vyeti vyake na Guinness World Recordsbaada ya kuweka rekodi kadhaa ikiwemo ya mwezi September katika mchezo dhidi ya Wolfsburg.

    Rekodi aliyoiweka Lewandowski mwezi September dhidi ya Wolfsburg ya kufunga goli 5 za haraka akitokea benchi, huku timu yake ya FC Bayern Munich ikiwa nyuma kwa goli 1-0 lakini alivyoingia yeye ndani ya dakika 9 akafunga goli tano na kubadili matokeo kuwa ya 5-1. November 30 akiwa uwanja wa mazoezi wa Bayern amekabidhiwa vyeti vyake vya rekodi nne kati ya tano.

    “Ulikuwa ni usiku wa kihistoria kwangu mimi, kwani ilinichukua siku na wiki nyingi kuweza kuweka rekodi hizi, familia yangu imefurahishwa na hili zaidi ya nilivyofurahia” >>> Lewandowski

    Hata hivyo Lewandowski ana jumla ya rekodi 5 zilizoingia katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records ambazo ni rekodi ya kufunga hat-trick ya mapema Ligi Kuu Ujerumani, kuongoza kwa kufunga goli nne za mapema katika historia ya Ligi Kuu Ujerumani, mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi akitokea benchi na rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga goli nyingi akitokea benchi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LEWANDOWSKI AINGIA KWENYE KITABU CHA MAAJABU YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top