728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, December 01, 2015

    CAZORLA AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUPIGA PASI 1000 EPL,HII HAPA 10 BORA


    London,England.

    KIUNGO wa Arsenal Muhispania Santi Cazorla ameonyesha kuwa yeye ni bingwa katika kupiga pasi baada ya kufanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka ligi kuu ya England kufikisha pasi 1,000 msimu huu.

    Kwa mujibu wa EA Sports Player Performance
    Index,Cazorla anaongoza akiwa amefanikiwa kupiga pasi 1,034 baada ya kucheza kwa dakika 1,204 zikiwa ni pasi 200 zaidi ya Andrew Surman wa Bournemouth anayefuatia akiwa amepiga pasi 812 baada ya kucheza kwa dakika 1,260.

    Nafasi ya tatu inashikwa na kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ambaye amepiga pasi 810 katika dakika ya 1,044 alizocheza msimu huu.

    Nafasi ya nne imekwenda kwa kiungo wa Manchester Fernandinho aliyepiga pasi 750 akitumia dakika 1,194,Mesut Ozil katika nafasi ya tano akiwa na pasi 732 katika dakika 1,117.

    Nyota wengine walio katika 10 bora ni:

    Gareth Barry pasi 717,Ashley Williams pasi 710, Glenn Whelan pasi 701,Simon Francis pasi 668 na Jonjo Shelvey pasi 667.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAZORLA AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUPIGA PASI 1000 EPL,HII HAPA 10 BORA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top