KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amekutana na hujuma ndani ya klabu hiyo baada ya kuundiwa zengwe la kutimuliwa pale atakapofungwa na Azam.
Simba na Azam zinatarajia kukutana wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Erick Onoka kutoka Arusha.
Habari kutoka ndani ya Simba zinasema Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji wa timu hiyo amegundulika kuanza kampeni za kuhakikisha Simba inafungwa katika mchezo huo ili kocha huyo aonekane hafai na kutimuliwa.
Chanzo hicho kilisema kuwa kiongozi huyo ameonesha wazi kutomtaka kocha huyo toka alipoanza kukinoa kikosi hicho.
"Kuna vitu anafanya kiongozi huyu ili mradi tu kocha atimuliwe kwa kuwa toka mwanzo alionyesha dhahiri hana uelewano naye,” kilisema chanzo hicho.
BINGWA lilimtafuta Rais wa Simba, Evans Aveva, kuzungumzia sakata hilo ambapo alisema wapo kwenye uchunguzi wa tuhuma hizo na hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika.
"Hizo tuhuma tumezisikia, sisi tunazifanyia kazi kama zikibainika basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake, hatuwezi kuwa na kiongozi wa aina hiyo, sisi tunatafuta ushindi yeye anatafuta matatizo," alisema Aveva.
Simba kwa sasa ipo kambini Zanzibar ikijiwinda na mechi yao dhidi ya Azam mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

(CHANZO:BINGWA)
0 comments:
Post a Comment