728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 10, 2015

    ISHU YA OKWI KURUDI SIMBA,UONGOZI WANENA


    SUALA la usajili wa mshambuliaji, Emmanuel Okwi, linaonekana kuwa ngumu kumeza kwa klabu ya Simba, kutokana na mambo mengi yaliyo nyuma ya pazia kwenye dili hilo.
    Ukiangalia uhusiano wa Simba na Okwi, utagundua kuwa mashabiki na viongozi wa klabu hiyo wanatamani sana kumuona staa huyo akiwa na jezi nyekundu kwa mara nyingine, lakini viongozi wanajikuta kwenye wakati mgumu kufanikisha dili hilo kutokana na gharama kubwa ambayo inatajwa kuambatana na usajili huo.
    Mganda huyo ambaye aliuzwa kwenye klabu ya SonderjyskE kwa dau la dola 120,000 (zaidi ya Sh milioni 250), huenda akaendelea kuwa stori ndani ya timu hiyo baada ya klabu hiyo kukumbwa na ukata wa kifedha.
    Awali klabu yake ya SonderjyskE ilitaka kumrejesha kwa mkopo Simba kwa miezi sita na baadaye dili hilo likakwama baada ya straika huyo kugoma kurejea Tanzania.

    Dili lake la kurejea Simba kwa mara nyingine huenda pia likakwama baada ya kiasi kikubwa kilichotajwa na klabu ya SonderjyskE kutaka warudishiwe fedha zao walizomnunua nyota huyo miezi sita iliyopita.
    Fedha hizo zinaonekana kuwa chungu kwa Simba kwa sasa kutokana na klabu hiyo kutokuwa na vyanzo vya mapato kiasi cha kushindwa kutekeleza mipango yao mbalimbali.

    Inajulikana Simba kwa msimu huu ilipanga mambo mbalimbali yakiwemo kuendeleza Uwanja wa Bunju, kufanya usajili wa maana sambamba na kushika nafasi tatu za juu vitu ambavyo vyote mpaka sasa vinaonekana kushindikana.
    Inajulikana wazi kuwa Simba kwa sasa haina fedha kiasi za kuilipa SonderjyskE ili kumpata mshambuliaji huyo kipenzi kwao.
    Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Haji Manara, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema bado klabu yao haijafanya mazungumzo yoyote na SonderjyskE.

    “Hatujafanya makubaliano yoyote mpaka sasa hivyo nashindwa kulizungumza suala la Okwi hasa kwenye kipindi hiki cha maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Azam,” alisema.

    (cHANZO:BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ISHU YA OKWI KURUDI SIMBA,UONGOZI WANENA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top