728x90 AdSpace

Sunday, December 13, 2015

MAKUNDI EURO YAPANGWA:ENGLAND USO KWA USO NA NDUGU ZAO WALES,FAHAMU MAKUNDI/VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA


Paris,Ufaransa.

Droo ya makundi ya michuano ya Ulaya (Euro 2016) imefanyika jana usiku kwa ndugu wawili England na Wales kutupwa kundi moja la B huku mwenyeji Ufaransa akipangwa kundi A pamoja na mataifa ya Romania,Albania na Uswisi.

 Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi lake nchini Ufaransa kuanzia Juni 10 mpaka Julai 10 ambapo jumla ya michezo 51 inatarajiwa kuchezwa katika viwanja 10.

Viwanja hiyo ni 

-Stade de Bordeaux, Bordeaux (42,000 capacity)
-Stade Bollaert Delelis, Lens Agglo (35,000)
-Stade Pierre Mauroy, Lille Metropole (50,100)
-Stade de Lyon, Lyon (58,000)
-Stade Velodrome, Marseilles (67,000)
-Stade de Nice, Nice (35,000)
-Parc des Princes, Paris (45,000)
-Stade de France, Saint-Denis (80,000)
-Stade Geoffroy Guichard, Saint-Etienne (41,500)
-Stadium de Toulouse Toulouse (33,000)

Fainali ya michuano hiyo itapigwa katika dimba la Stade de France,ambalo lilichezewa fainali ya kombe la dunia la mwaka 1998 na wenyeji Ufaransa kuibwaga Brazil kwa mabao 3-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MAKUNDI EURO YAPANGWA:ENGLAND USO KWA USO NA NDUGU ZAO WALES,FAHAMU MAKUNDI/VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown