728x90 AdSpace

Sunday, December 13, 2015

CHICHARITO APIGA HAT TRICK,LEVERKUSEN IKISHINDA TANO MTUNGI

Leverkusen,Ujerumani.

Javier Hernandez "Chicharito" ameendelea kuionyesha Manchester United kuwa ilikosea kumpiga bei baada ya leo hii kuifungia Bayer Leverkusen magoli matatu (hat-trick) ndani ya dakika 13 katika ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mchezo wa ligi ya Bundesliga uliopigwa katika dimba la BayArena.

Chicharito amefunga magoli hayo dakika za 63,74 na 76 na kufikisha magoli 15 katika michezo 12 ya ligi ya Bundesliga.Magoli mengine ya Bayer Leverkusen yamefungwa na Stefan Kiessling aliyefunga mara mbili na kuhitimisha safari ndefu ya Borussia
Monchengladbach ambayo ilikuwa haijapoteza mchezo wowote msimu huu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: CHICHARITO APIGA HAT TRICK,LEVERKUSEN IKISHINDA TANO MTUNGI Rating: 5 Reviewed By: Unknown