Bournemouth,England.
Bournemouth imeendelea kuwa tishio kwa vigogo baada ya leo kuitandika Manchester United kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu nchini England uliopigwa katika dimba la Vitality.
Bournemouth ambayo wiki iliyopita iliizidi ujanja Chelsea na kuibwaga kwa bao 1-0,leo ilianza mapema kuonyesha dalili ya ushindi dhidi ya Manchester United baada ya kupata bao la kuongoza dakika ya 1 tu ya mchezo kupitia kwa Junior Stanislas na kisha la pili dakia ya 54 kupitia kwa Josh King akizima bao la Marouane Fellaini aliloifungia Manchester United dakika ya 24.
Kufuatia ushindi huo mkubwa Bournemouth imefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 16.Mara ya mwisho Bournemouth kuifunga Manchester United ilikuwa ni kwenye michuano ya kombe la FA la mwaka 1984.
0 comments:
Post a Comment