Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Yaya Toure leo ameibuka kidedea baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika wa BBC kwa mwaka 2015.
Toure ameitwaa tuzo hiyo akiwabwaga Yacine Brahimi wa Algeria mshindi wa mwaka 2014 na Pierre-
Emerick Aubameyang wa Gabon,Andrew Ayew wa Ghana pamoja na nyota wa Senegal Sadio Mane kufuatia kuiwezesha Ivory Coast kutwaa ubingwa wa Afrika mwezi Februari huku akiiwezesha Manchester City kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya England msimu uliopita.
Toure,32 ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kutwaa tuzo hiyo mara mbili akiungana na Jay Jay Okocha na Nwankwo Kanu mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment