Farid Mussa.
Dar es salaam,Tanzania.
Nyota wawili wa mabingwa wa kombe la Kagame Azam FC Farid Mussa na Himid Mao wanatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kuanzia sasa kwenda nchini Ubelgiji kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Akiongea na kipindi cha Sports Leo cha Radio One Sterio Afisa habari wa klabu hiyo Jaffar Iddy Maganga amethibisha Azam FC kupokea taarifa rasmi ya nyota hao kutakiwa nchini Ubelgiji lakini hakutaja jina la klabu husika.
Ameongeza nyota hao wanatakiwa haraka nchini Ubelgiji hivyo kuna uwekano mkubwa wakaukosa mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho dhidi ya Esperance Aprili 20.
Wakati huohuo Jaffar Iddy Maganga amesema mlinzi wa klabu hiyo Shomary Kapombe anaendelea vizuri na matibabu nchini Afrika Kusini alikokwenda wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment