Milan,Italia.
Klabu ya AC Milan imemtimua kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Mserbia Sinisa Mihajlovic.
Uamuzi huo wa kumtimua kazi Mihajlovic,47 umekuja baada ya AC Milan kushindwa kupata ushindi katika michezo mitano iliyopita ya ligi ya Seria A.
AC Milan inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya Seria A ikiwa pointi saba nje ya mstari wa kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa
Ligi.
Wakati huohuo taarifa zinasema AC Milan tayari imemteua nyota wake wa zamani Cristian Brocchi kuwa kocha wake wa muda mpaka mwisho wa msimu.
Brocchi,40 anakuwa kocha wa tano kuinoa AC Milan katika kipindi kisichozidi miaka mitatu.
0 comments:
Post a Comment