Bournemouth, England.
Klabu ya Bournemouth imeongeza makali katika idara yake ya ushambuliaji baada ya jana jumapili kumsajili straika wa zamani wa Arsenal Benik Afobe kwa dau la £12m akitokea klabu ya daraja la kwanza ya Wolverhampton Wanderers.
Afobe,22 aliyeachana na Arsenal miezi 18 iliyopita na kutua Wolverhampton Wanderers kwa dau la £1.8m anakuwa mchezaji ghari zaidi kuwahi kusajiliwa na Bournemouth akivuka dau la £8m lililotolewa mwaka 2015 kumsajili Tyrone Mings toka Ipswich Town.
Afobe amejiunga na Bournemouth kwa mkataba wa miaka minne na nusu baada ya kuifungia Wolverhampton Wanderers magoli 23 katika michezo 48 huku msimu huu akifunga jumla ya magoli tisa
0 comments:
Post a Comment