728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 09, 2016

    LIVERPOOL YABANWA EMIRATES FA CUP,YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA EXETER CITY

    Exeter,England.

    Liverpool imeshindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na klabu ya daraja la pili ya Exeter City katika mchezo wa raundi ya tatu wa michuano ya Emirates FA Cup uliopigwa katika dimba la St.James Park huko Exeter ijumaa usiku.

    Exeter City ikiwa mbele ya watazamaji 8,298 ilipata mabao yake dakika za 9 na 45 kupitia kwa Tom Nichols na Matt Holmes huku Liverpool ambayo sehemu kubwa ya kikosi chake kiliundwa na vijana ikijibu dakika za 12 na 73 kupitia kwa Jerome Sinclair na Brad Smith.

    Kufuatia sare hiyo Liverpool na Exeter City zitarudiana tena Anfield hapo baadae kupata timu moja itakayotinga hatua inayofuata.

    Vikosi

    Exeter City:Bobby Olejnik;
    Christian Ribeiro, Troy Brown, Jordan Moore-Taylor, Craig Woodman; Jordan Tillson; Alex Nicholls, David Noble, Matt Holmes; Tom Nichols, Jamie Reid.

    Liverpool: Adam Bogdan; Connor Randall, Tiago Ilori, Jose Enrique, Brad Smith;
    Joao Teixeira, Kevin Stewart, Cameron Brannagan, Ryan Kent; Jerome Sinclair,Christian Benteke.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIVERPOOL YABANWA EMIRATES FA CUP,YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA EXETER CITY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top