BERLIN,UJERUMANI.
Timu ya taifa ya Ivory Coast imepata pigo baada ya mlinzi wake wa zamani Steve
Gohouri kukutwa amekufa katika mto Rhine ulio katika mji wa Krefeld,kaskazini magharibi mwa Duesseldorf.
Kifo cha Gohouri,34 kimekuja zikiwa ni siku chache tu tangu familia yake itangaze kuwa nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Wigan, Young Boys na Paris Saint-Germain,Maccabi Tel Aviv na Borussia Moenchengladbach amepotea.
Desemba 21 familia ya Gohouri iliamua kutangaza kupotea kwa nyota huyo baada ya jitihada za kumpata kugonga mwamba kufuatia nyota huyo kushindwa kukuungana nayo jijini Paris kusherekea sikukuu ya Krismasi.Kabla ya hapo Gohouri alikuwa katika pati ya Krismasi na klabu yake ya TSV Steinbach.
SAFARI YAKE YA SOKA
Gohouri aliichezea Ivory
Coast kati ya mwaka 2006 na 2009 na kufanikiwa kuifungia magoli matatu katika michezo 13 ya kimataifa.
Mwaka 2008 aliipandisha daraja Borussia
Moenchengladbach huku akifanikiwa kuifungia magoli mawili katika michezo 42.
Mpaka kifo kinamchukua Gohouri alikuwa akiichezea klabu ya TSV Steinbach inayoshiriki ligi daraja la nne nchini Ujerumani.Mpaka tunakwenda mitamboni chanzo cha kifo hicho kilikuwa bado hakijafahamika.
0 comments:
Post a Comment