Bogota,Colombia.
Mlinda mlango wa zamani wa timu ya taifa ya Colombia Faryd Mondragon yuko mahututi hospitalini baada ya jaribio lake la kutaka kujiua kushindikana.
Mlinda mlango huyo aliyewahi kuchezea vilabu vya Galatasaray na Metz amelazwa katika hospitali ya Fundacion Valle del Lili iliyoko Cali,Colombia baada ya kupata tatizo liitwalo "metabolic imbalance" lililotokana na kunywa vidonge vingi zaidi.
Mondragon ambaye mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 43 aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kucheza kombe la dunia pale alipoingia kuchukua nafasi ya David Ospina katika mchezo ambao 43 Colombia iliifunga Japan kwa mabao 4-1 mapema wiki hii aliandika ujumbe wenye utata katika mtandao wa kijamii ujumbe ambao umefutwa baada ya tukio la kutaka kujiua.
Ujumbe huo ulisema hivi "Mimi pekee ndiye mwenye uwezo wa kuhukumu maisha yangu.Nimechoka kuhukumiwa na watu wengine bila ya kupewa nafasi ya kujitetea".Polisi wameanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment