London,England.
Bao la dakika ya 72 la mlinzi Laurent Koscielny limeipa Arsenal ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Emirates.
Kufuatia ushindi huo Arsenal imeendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu England baada ya kufikisha pointi 42 baada ya kushuka dimbani mara 20.
Katika mchezo mwingine Manchester United ikiwa nyumbani Old Trafford imeifunga Swansea City kwa mabao 2-1.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Antony Martial dakika ya 46 na Wayne Rooney dakika ya 70 huku Glylif Sirgudsson akiipatia Swansea City bao la kufutia machozi dakika ya 77.
Kufuatia ushindi huo Manchester United imepanda mpaka nafasi ya tano baada ya kufikisha pointi 33 baada ya kucheza michezo 20.
Matokeo mengine
Sunderland 3-1 Aston Villa
Leceister City 0-0 Bournemouth
Norwich City 1-0 Southampton
Westham 2-0 Liverpool
0 comments:
Post a Comment