London,England.
CHUPU CHUPU!!Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kutumia kulielezea tukio la jana alhamis la nyota wawili wa Chelsea Diego Costa na Oscar Dos Santos kutaka kugombana baada ya kuchezeana rafu mazoezini wakati wa maandalizi ya mchezo wa kombe la FA jumamosi dhidi ya Scunthorpe United utakaopigwa katika dimba la Stamford Bridge.
Kisa cha ugomvi huo kimedaiwa kuwa ni kulipizana visasi.Inadaiwa Costa alimchezea rafu mbaya Oscar kisha muda mfupi baadae Oscar akajibu kwa kumkanyaga gotini Costa ambaye alikuja juu akamkwida na kutaka kurushia ngumi kabla ya kuamulia na wachezaji wenzao.
Tukio hili ni la pili kuikumba Chelsea baada ya mapema mwezi uliopita Charly Musonda na Cesc Fabregas nao kuwa karibu kugombana baada ya Fabregas kukasirika kufuatia kupigwa tobo na Musonda.
0 comments:
Post a Comment