728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 01, 2016

    KIBALI CHAKWAMISHA USAJILI WA ELNENY ARSENAL

    London,England.

    Licha ya kuripotiwa kufuzu vipimo vya afya pamoja na kukamilisha makubaliano binafsi juu ya mshahara na masuala mengine kiungo Mmisri Mohamed Elneny huenda akachelewa kujiunga na Arsenal baada ya kukwama kupata kibali cha kufanyia kazi nchini England.

    JE,SABABU NI NINI??

    Kwa mujibu wa sheria mpya za chama cha soka cha England FA ni kuwa mchezaji anayetoka nje ya nchi za umoja wa Ulaya ni lazima taifa lake liwe katika nafasi 50 za juu katika orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani badala ya nafasi 70 kama ilivyokuwa zamani.

    Hivyo kutokana na sheria hiyo mpya Elneny amekosa sifa ya kucheza ligi kuu nchini England kwani kwa sasa Misri inashika nafasi ya 57 katika orodha ya viwango vya soka duniani.Pia bado hajafikisha asilimia hamsini za kuichezea Misri katika michuano ya kimataifa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

    JE,ARSENAL WANAPASWA KUFANYA NINI?

    Arsenal hawapaswi kusitisha mpango wa kumsajili Elneny bali wanapaswa kukata rufa FA na kutoa ushahidi utakaokuwa na mashiko juu ya uwezo wa nyota huyo licha ya kukosa vigezo tajwa hapo juu.

    Hali kama hii ilishawahi kumpata raia mwingine wa Misri Mohamed Salah mwaka 2013 alipokuwa akitaka kuhamia Chelsea lakini baada ya kukatiwa rufaa FA alipewa kibali.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIBALI CHAKWAMISHA USAJILI WA ELNENY ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top