London,England.
Mshambuliaji Alexander Pato amejiunga na Chelsea kwa mkopo wa miezi sita akitokea Corinthias ya nyumbani kwao Brazil.
Pato,26 aliyewahi kutamba na Ac Milan ya Italia amekuwa ni Mbrazil wa 67 kujiunga na klabu ya ligi kuu England baada ya Mirandinha kuweka historia ya kuwa Mbrazil wa kwanza kucheza ligi kuu England baada ya kusajiliwa na Newcastle mwaka 1987.
Wakati huohuo Chelsea iko karibu kuinasa saini ya mlinzi mwenye miaka 20 Matt Miazga toka New York Red Bulls ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment