Zanzibar
Yanga imeanza michuano ya Mapinduzi kwa kishindo kwa kuitwanga Mafunzo kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo.
Mabao mawili ya Yanga yamefungwa na Donaldo Ngoma aliyepewa pasi na
Mzimbabwe mwenzake Thabani Kamusoko katika dakika za 31 na 34 na
kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili, Mafunzo walijitutumua na kupeleka mashambulizi kadhaa
likiwemo lililozaa penalti baada ya Kelvin Yondani kuachwa na kumvuta
mshambuliaji wa Mafunzo, lakini kipa Deo Munishi ‘Dida’ akaipangua na baadaye kuidaka.
Paul Nonga aliyeingia dakika 10 za mwisho kuchukua nafasi ya Tambwe alifunga bao la tatu katika dakika ya 90 huku walinzi wa Mafunzo wakiamini alikuwa ameotea.
0 comments:
Post a Comment